Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yawasaidia watoto kurudi shuleni Yemen

UNICEF yawasaidia watoto kurudi shuleni Yemen

Mzozo unaoendelea nchini Yemen umekuwa na athari kubwa kwa sekta ya kibinadamu na fursa ya mamilioni ya watoto kupata elimu.Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa Grace)

Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF Kufuatia miezi ya vurugu na vita mijini imesababisha zaidi ya shule 3,600 kufungua na kupelekea wanafunzi na familia zao kuhamia maeneo salama nchini Yemen.

Karibu shule 248 zimepata uharibifu wa moja kwa moja huku shule 270 zikihifadhi wakimbizi wa ndani na shule 68 zikikaliwa na makundi yaliyojihami

Kwa mantiki hiyo UNICEF inaendesha darasa maalum la kuwawezesha wanafunzi kupata masomo waliyokosa.

Christophe Boulierac ni msemaji wa UNICEF mjini Geneva

“ Watoto milioni 1.8 hawakwenda shuleni kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili, na hata kabla ya mzozo, watoto milioni 2 walikuwa hawaendi shuelni. Inatia moyo sana ukiona watoto wanavyotaka kusoma wakati kuna mapigano, hakuna chakula, hakuna umeme, hakuna karatasi. Kwa hiyo wametutumia ujumbe huo, na sisi tunajaribu kujitahidi kwenye mazingira haya magumu.”