Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yakaribisha tathimini ya chanjo ya malaria

WHO yakaribisha tathimini ya chanjo ya malaria

Shirika la afya uliwenguni WHO limekaribisha tathmini chanya ya chanjo dhidi ya malaria iliyofanywa na shirika la dawa barani Ulaya EMA,  na kueleza kuwa hiyo ni hatua muhimu katika maendeleo ya chanjo dhidi  ya ugonjwa huo na namna itakavyotumika.WHO imesema kuwa tathmini ya EMA sio mapendekezo ya kutumia chanjo na kwamba shirika hilo la afya  litatoa mapendekezo yake ya matumizi mwezi Novemba mwaka huu licha ya kwamba chanjo hiyo yaweza kuanza kutumika mwaka 2017.

Sera ya mapendekezo ya WHO inazingatia  vigezo kadhaa vinavyoelezwa na mamlaka za kudhibiti utolewaji wa chanjo ambapo Gregory Härtl afisa mahusiano ya umma anaeleza hatua muhimu za kuchukau sasa.

(SAUTI )

‘‘Upembuzi wa kutumia chanjo hii kwa jamii katika nchizinazoendelea, tunahitaji kuangalia namana ya kuendesha chanjo na ufanisi wa  garama zake. ‘’