Vijana wa Tanzania washindi wa tuzo ya lugha za kigeni ya UN

Vijana wa Tanzania washindi wa tuzo ya lugha za kigeni ya UN

Utamaduni na Elimu

Lugha ya kigeni ni hati ya kusafiria kwenda kwingineko! Hilo limedhihirika hii leo.

Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani leo, vijana 70 kutoka nchi 42 tofauti duniani wameshiriki katika hafla maalum iitwato “lugha nyingi, dunia moja” iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuleta mabadiliko katika elimu duniani yaani United Nations Academic impact kwa ajili ya kukuza ujuzi wa lugha miongoni mwa vijana duniani.

Vijana hawa 70 ni washindi wa mashindano yaliyofanyika mwaka huu yenye lengo la kuandika insha kuhusu ajenda ya maendeleo ya baada ya mwaka 2015 katika lugha ya kigeni kwao.

Collins Maringa na Emmanuel Manko ni watanzania wanaosoma nchini Algeria. Wameandika insha yao kwa lugha ya kifaransa. Emmanuel anaeleza zaidi.

(Sauti ya Emmanuel) 

Kwa upande wake Collins anafafanua umuhimu wa kuzungumza lugha za kigeni.

(Sauti ya Collins)