Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhu ya mataifa mawili mashariki ya kati inakufa pole pole : Baraza la Usalama

Suluhu ya mataifa mawili mashariki ya kati inakufa pole pole : Baraza la Usalama

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa utaratibu wa amani Mashariki mwa Kati, Nickolay Mladenov ameeleza wasiwasi wake leo kuhusu ongezeko ka misimamo mikali na ghasia kwenye ukanda huo, huku mazungumzo ya amani baina ya Israel na Palestina yakiwa yamesitishwa.

Amesema hayo kwenye kikao cha mwezi cha Baraza la Usalama kuhusu swala la Palestina, akisikitishwa na kuona kwamba hali hiyo inatishia uwezekano wa kuwepo tena kwa suluhu ya mataifa mawili.

Bwana Mladenov amezisihi mamlaka za Israel kusitisha ujenzi wa ukoloni kwenye maeneo yaliyotawaliwa ya Palestina, aidha kutoendelea kubomoa nyumba na kufukuza wakazi.

Halikadhalika, ameziomba mamlaka za Palestina kujitahidi kurejesha umoja baina yao na kundi la Hamas linalotawala Gaza.

(SAUTI MLADENOV)

« Muda umefika sasa kuchukua hatua za maana ili kubadilisha mtazamo unaozidi kukuwa siku hizi kwamba suluhu ya mataifa mawili inaanza kufa pole pole ikiwa na vidonda elfu moja. »