Mkuu wa UN nchini Somalia akaribisha uteuzi wa Rais wa Galmudug

23 Julai 2015

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay, amekaribisha uteuzi wa Abdikarim Hussein Guled kama Rais wa mamlaka mpya ya mpito ya Galmudug, Galmudug Interim Administration (GIA).

Akizungumza kwenye hafla maalum iliyofanyika Adaado, mkoani humo, Bwana Kay amepongeza rais Guled na Naibu wake Mohamed Hashi Abdi kwa kuchaguliwa na bunge la Galmudug ili wajenge mamlaka za mkoa huo na kuhakikisha usalama wa eneo hilo.

Amezisihi serikali kuu ya Somalia na serikali ya GIA kuwasiliana ili kushirikiana kwa amani pamoja na kundi la Ahlu Sunnah Wal Jama’a na serikali ya Puntland.

Mkoa wa Galmudug umetangaza kujitawala mwaka 2006, huku ukisema kuwa tayari kushirikiana na serikali kuu ya Somalia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter