Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yapambana na utapiamlo Nepal

UNICEF yapambana na utapiamlo Nepal

Kufuatia matetemeko ya ardhi yaliyoathiri Nepal mwezi wa nne mwaka huu, nakuleta athari kadhaa zikiwamo ukosefu wa chakula,  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limeanzisha mradi wa kupambana na utapiamlo nchini humo.Katikati mwa nchi, kwenye wilaya zilizoathirika zaidi na janga, UNICEF inapima uzito wa watoto na kuwapatia chakula maalum.

Vipimo vilivyofanyika vimeonyesha kwamba utapiamlo ulikuwa ukikumba familia nyingi hata kabla ya matetemeko ya ardhi.

Kulikoni?

Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.