Skip to main content

Haki za binadamu muhimu katika kupambana na wapiganaji wanaovuka mipaka

Haki za binadamu muhimu katika kupambana na wapiganaji wanaovuka mipaka

Pamoja na kuwa wapiganaji wanovuka mipaka na kujihusisha na vitendo vya  kigaidi ni hatari duniani lakini mataifa yanapaswa kuzingatia sheria za kimataifa za haki za binadamu katika kukabiliana nao .

Hii ni kauli ya wajumbe wa kikundi kazi kuhusu mamluki kilichoko chini ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambacho mwaka huu kinamulika Wapiganaji wanaovuka mipaka.

Wajumbe hao Bi Elzbieta Karska, na Bwana Gabor Rona wamewaambia waandishi  wa habari mjini New York kuwa mada hiyo watakayoiwakilisha katika ripoti yao kwenye kikao cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa inakumbana na mambo mengi magumu ikiwamo uvunjifu wa sheria za kimataifa za kibinadmau na haki za binadamu kutoka kwa nchi ambazo Rona anasema husababisha.

(SAUTI RONA)

‘‘Inahatarisha ukosefu wa haki za kujieleza,haki ya kushiriki katika michakato ya kisiasa, haki ya faragha, na pia haki ya kutowekwa kizuizini na uteswaji.’’

Kwa upande wake Bi Karska amesema kikundi kazi hicho kinajaribu kutoa maana halisi ya mamluki ili kuondoa mkanganyiko katika kuanisha dhana hiyo  na pia kutoa mapendekezo ya namna  ya kukabilana na wapiganaji wanaovuka mipaka.