Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Marekani yatoa dola milioni 13 kwa UNRWA

Serikali ya Marekani yatoa dola milioni 13 kwa UNRWA

Serikali ya Marekani imetoa mchango wa kiasi cha dola milioni 13 kusaidia wakimbizi wa Palestina waliotahiriwa na mzozo wa Syria.

Marekani ambayo ni nchi inayoongoza kwa kiwango kikubwa cha mchango kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia wakimbizi wa Palestian UNRWA, kupitia mchango huu limefikisha kiasi cha dola 76.4 kwa mwaka huu 2015 .

Taarifa ya UNRWA kuhusu changizo hilo imemnukuu kamishna wa shirika hilo Pierre Krähenbühl akisema madhara ya miaka minne ya mzozo yanaonyesha kuwa Syria kwa sasa ina hali mbaya zaidi huku fedha za kushugulikia hata mahitaji ya msingi yakisailia changamoto.

Kamishina Krähenbüh amesihukuru serikali ya Marekani kwa mchango wake nakusema kuwa dola milioni 9.1 ya mchango huo utatumika katika kazi za kibiandamu za UNRWA nchini Syria ambapo asilimia 95 ya wakimbizi 480,000 ya Kipalestina walioko nchini humo wanategemea shirika hilo kwa mahitaji kama vile chakula, malazi, maji na huduma za usafi.