Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzalishaji wa chakula waongezeka Syria, usalama wa chakula bado shakani: Ripoti

Uzalishaji wa chakula waongezeka Syria, usalama wa chakula bado shakani: Ripoti

Uzalishaji wa chakula nchini Syria umeongezeka mwaka huu kutokana na mvua lakini mgogoro unaoendela unazidi kuongeza kiwango cha njaa na umasikini. Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa leo na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa. Taarifa kamili na John Kibego.

(TAARIFA YA KIBEGO)

Mashirika hayo lile la chakula na kilimo FAO na lile la mpango wa chakula duniani WFP yanasema katika ripoti yao yao ya pamoja kuwa uzalishaji wa nafaka mathalani ngano kwa mwaka huu wa 2015 utaongezeka ukilinganishwa na mwaka jana lakini hautaongeza usalama wa chakula kwa ujumla nchini Syria

Ripoti pia inaweka bayana kuwa kwa ujumla watu milioni tisa nukta nane wanakadiriwa kutokuwa na usalama wa chakula hukumilioni sita nukta nane kati yao wakikumbwa na njaa kali hatua ambayo inahitaji msaada wa chakula kutoka nje ya taifa hilo.

Dominique Burgeon ni Mkurugenzi wa dharura na uragibishaji wa FAO

(SAUTI DOMINIQUE)

‘‘Kilimo nchini Syria kinaendelea kuathiriwa na ukosefu wa mafuta, mbegu bora na ukosefu wa pembejeo kama mbolea.’’

Tangu mwezi Januari watu milioni moja wamepoteza makazi nchini Syria kutoakana na mzozo unaoendelea.