Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa UM wasifu hatua ya Zambia kuachana na hukumu ya kifo

Wataalam wa UM wasifu hatua ya Zambia kuachana na hukumu ya kifo

Wataalam wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, wameikaribisha hatua ya rais wa Zambia, Edgar Lungui, ya kubadilisha hukumu za kifo kwa watu 332 kuwa vifungo vya maisha.

Mtaalam maalum kuhusu mauaji kiholela, Christof Heyns na yule anayehusika na utesaji, Juan E. Méndez, wamehimiza mamlaka za Zambia kwenda hatua hata zaidi na kuondoa kabisa hukumu ya kifo katika sheria za taifa hilo.

Wataalam hao wamesema kwa kuondokana na hukumu ya kifo, Zambia imekomesha uchungu wa kiakili na kimwili kwa wafungwa, na hivyo kuchukua hatua muhimu katika kuhakikisha heshima kwa utu wa mwanadamu.

Hata hivyo, wameonya kuhusu kuendelea kuwepo hofu ya hukumu ya kifo katika baadhi ya nchi barani Afrika, kama vile Misri ambako wakati mwingine hukumu ya kifo inatolewa kwa halaiki ya watu.