Skip to main content

Conakry yateuliwa na UNESCO kuwa mji mkuu wa kitabu duniani 2017

Conakry yateuliwa na UNESCO kuwa mji mkuu wa kitabu duniani 2017

Mji mkuu wa Guinea, Conakry, umeteuliwa kuwa mji mkuu wa Kitabu Duniani kwa mwaka 2017.

Uteuzi huo umefanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO kufuatia chaguo la kundi la wataalam waliokutana mjini Paris, Ufaransa.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo na UNESCO, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova amenukuliwa akisema vitabu ni ufunguo kwenye maisha na jitihada za serikali ya Guinea katika kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika zinaonyesha dira ya nchi inayoangazia utamaduni na elimu kama misingi ya maendeleo.

Mji Mkuu wa kitabu duniani huchaguliwa kila mwaka na mashirika ya kimataifa yanayohusika na uzalishaji wa vitabu pamoja na UNESCO, mwaka huu ukiwa ni mji wa Incheon, nchini Korea na mwaka kesho Wroclaw, nchini Poland.