Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zote, kila sekta kujumuishwa kwenye ajenda ya maendeleo baada ya 2015: Kamau

Nchi zote, kila sekta kujumuishwa kwenye ajenda ya maendeleo baada ya 2015: Kamau

Majadiliano ya siku tano  baina ya seriakali kuhusu ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 yanaendelea  hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo mpango wa mwisho wa kazi ya kuandaa malengo ya maendeleo endelevu (SDGS) ulioanza miaka mitatu iliyopita unakamilishwa.

Katika mahojiano na idhaa hii kandoni mwa majadiliano hayo Mwenyekiti wa kikundi kazi  katika kuratibu SDGS ambaye ni mwakilishi wa kudumu wa Kenya katika ofisi ya Umoja wa Mataifa, balozi Macharia Kamau anaeleza matarajio ya dunia katika ajenda hiyo.

(SAUTI KAMAU)

Amesisitiza kuwa ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 imezingatia nchi zote tofauti na malengo ya maendeleo ya milenia (MDGS) ambayo yalilenga zaidi kuinua nchi masikini.