Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNESCO apewa tuzo na rais wa Mali

Mkuu wa UNESCO apewa tuzo na rais wa Mali

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, amepokea tuzo ya hadhi ya heshima kutoka kwa rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keïta.

Akimkabidhi tuzo hiyo, Rais Keïta amesema ametambua mchango wake katika kulinda urithi wa mji wa kihistoria wa Timbuktu, akiongeza kuwa Mali ina moyo unaotaka amani, katika ulimwengu ambao mara nyingi hukataa kufuata mkondo wa amani.

Akiipokea tuzo hiyo, Bi Bokova amesema inampa moyo hata zaidi, akiongeza kuwa anaona fahari kuipokea kwa niaba ya UNESCO. Amesema UNESCO itaendelea kushirikiana na Mali katika kuulinda urithi wake, na kuhakikisha kuna elimu bora kwa wote.