Naibu mpya wa Mwakilishi wa UM Somalia awasili Mogadishu

20 Julai 2015

Naibu mpya wa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Peter de Clergq, amewasili leo mjini Mogadishu ili kuanza majukumu yake katika ofisi hiyo.

Bwana de Clercq ambaye ni raia wa Uholanzi, atakuwa pia Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa, Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu, na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP.

Bwana de Clercq ana uzoefu mkubwa katika kusimamia michakato ya kisiasa, maendeleo ya sekta ya usalama, operesheni za dharura, ulinzi wa raia na utawala wa sheria, pamoja na kuchagiza na kusimamia misaada ya kibinadamu na misaada ya maendeleo.

Aliwahi kufanya kazi nchini Somalia pia, kama Mshauri Mkuu wa Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Naibu wa Mwakilishi Maalum wa Ofisi ya Masuala ya Kisiasa Somalia, UNPOS, kati ya 2012 na 2013.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter