Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani yaimarika Burundi licha ya kuuliwa kwa mkimbizi: Mbilinyi

Amani yaimarika Burundi licha ya kuuliwa kwa mkimbizi: Mbilinyi

Hali ya amani inaimarika nchini Burundi hususani  kwa wakimbizi kutoka nchi jirani  waliojihifadhi nchini humo licha ya taarifa za kifo cha mkimbizi  mmoja ambaye sababu za kifo chake imeelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR kuwa haitokani na ghasia za kisiasa.

Mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini Burundi Abel Mbilinyi ameiambia idhaa hii katika mahojiano kuwa baada ya uchunguzi wa tukio hilo imegundulika kuwa mkimbizi huyo aliyekuwa akifanya kazi katika duka la kubadilishia fedha aliuwawa katika tukio la ujambazi.

Bwana Mbilinyi anafafanua zaidi tukio hilo na kutoa wito kwa wakimbizi na jumuiya ya kimataifa.

(SAUTI MBILINYI)