Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chukua hatua hamasisha mabadiliko katika siku ya Mandela: Ban

Chukua hatua hamasisha mabadiliko katika siku ya Mandela: Ban

 

Raia kote ulimwenguni wametakiwa kuiga mfano wa ushawishi wa uthabiti wa Mandela wa huduma kwa watu. Huu ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika siku ya kimataifa ya Mandela July 18 kila mwaka.Sherehe hizi za kila mwaka mnamo Julai 18 huadhimisha kuzaliwa kwa Rais wa kwanza wa Afrika Kusini aliyechaguliwa kwa njia ya demokrasia ambaye alifariki miaka miwili iliyopita akiwa na miaka 95.

Katibu Mkuu amemweleza Nleson Mandela kama kiongozi aliyeamini daima katika haki na usawa wa binadamu.Amesema dhima ya siku ya kimataifa ya Mandela chukua hatua, hamasisha mabadiliko inamulika umuhimu wa kufanya kazi pamoja kujenga dunia ya  amani, uendelevu na yenye usawa.

Bwana Ban amesema Mandela alitumia miaka 67ya maisha yake kupigania haki za binadamu na haki ya jamii. Katika kumenzi kiongozi huyo anayefahamika pia kwa jina la Madiba, watu duniani kote wanatakiwa kutumia dakika 67 kufanya kazi za kijamii katika siku hii ya kuzaliwa kwake.

Umoja wa Mataifa utatawaza tuzo ya heshima kwa jina la Mandela badaye mwezi huu. Dk Helena Ndume daktari wa macho kutoka Namibia na Raisi wa zamani wa Ureno Jorge Sampaio, watakuwa wa kwanza  kupokea tuzo hiyo. Tuzo hiyo iitwayo Nelson Rolihlahla Mandela itatolewa kila baada ya miaka mitano kwa mwanamme na mwanamke ambao kazi zao zimejengwa katika misingi ya maisha ya Mandela.