Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili dhidi ya wazee na namna ya kuwakwamua

Ukatili dhidi ya wazee na namna ya kuwakwamua

Leo ikiwa ni mapumizko hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kwa jaili ya kiadhimisha sikukuu ya Idi Elfitri tunakuletea jarida maalum kuhusu wazee na haki zao.

‘‘Ukatili dhidi  ya wazee mara nyingi hutokea kwa kificho. Paza sauti hadharani ili jamii ikusikie, hili ni muhimu’’. Hii ni kauli ya karipio kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa   Ban Ki-moon ambaye anaitaka jamii kuinuka dhidi ya ukatili unaotendwa kwa wazee ili kuleta maisha yenye utu kwa wote.

Kwa kutambua umuhimu wa kundi hili, ustawi na hata ulinzi wazee ambao kwa mujibu wa takwimu za UM ifikapo mwaka 2025 idaidi ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 itakuwa mara mbili kutoka idadi ya mwaka 1995 ya bilioni 1.2 . Takwimu zinasema takribani asilimia nne hadi sita  ya wazee wamekumbana na ukatili majumbani. Ukatili huo unaweza kusababisha majeruhi makubwa na madhara ya muda mrefu ya kisaikolojia.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupitia azimio lake nambari 66/127 limepitisha siku ya Juni 15 kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya kuhamasisha kupinga ukatili dhidi ya wazee. Siku hii inataka haki za kundi hili zidumishwe ikiwamo haki ya kuapata matiababu na huduma nyingine za kijamii.

Kufahamu hali ilivyo Afrika Mashariki tunaanzia nchini Uganda ambapo John Kibego anasimulia adha wanazokumbana nazo wazee.

(PACKAGE KIBEGO)