Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA yajizatiti kutokomeza ndoa za utotoni Tanzania

UNFPA yajizatiti kutokomeza ndoa za utotoni Tanzania

Ndoa za utotoni huelezwa na wataalamu wa afya kuwa sio tu huathiri afya kutokana na miili ya watoto hao kutokuwa tayari , bali pia huleta athari za muda mrefu za kisaikolojia. Nchini Tanzania wadau wa afya ya uzazi wakiongozwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu UNFPA wanaelimisha na kuchukua hatua stahiki dhidi ya kitendo hicho.

Ungana na Grace Kaneiya katika makala itakayokupa simulizi za kusikitisha za wasichana waliopewa mimba katika umri mdogo.