Mapigano yazuka kaskazini mwa Darfur: UNAMID

16 Julai 2015

Ujumbe wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa jimboni Darfur nchini Sudan UNAMID umeripoti taarifa za kukua kwa mapigano kaskazini mwa nchi kulikochochewa na wizi wa mifugo.

Kwa mujibu wa msemaji wa Katibu Mkuu wa UM Stéphane Dujarric, UNAMID imeyataka makabila katika mzozo huo ambayo ni Rizeigat na Habaniya kufanya majadiliano ili kutatua mzozo huo na pia.

(SAUTI DUJARRIC)

‘‘Kujizuia katika vitendo vyote vinavyoweza kusababisha kukua kwa mgogoro, vifo na ukosefu wa makazi.’’

Amewaambia waandishi wa habari kuwa UNAMID inafuatilia kwa karibu mgogoro huo na kutoa usaidizi katika juhudi za kuzuia kuendelea kwa mapigano.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter