Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makubaliano ya Addis ni hatua muhimu katika kujenga ulimwengu wa ufanisi na utu kwa wote- Ban

Makubaliano ya Addis ni hatua muhimu katika kujenga ulimwengu wa ufanisi na utu kwa wote- Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amezipongeza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa kuafikia ajenda ya Addis Ababa ya kuchukua hatua, ambayo ni matokeo ya kongamano la tatu la ufadhili kwa maendeleo.

Bwana Ban ameitaja ajenda hiyo ya kuchukua hatua iliyopitishwa hapo jana Alhamis kama hatua muhimu katika kujenga ulimwengu wenye ufanisi na utu kwa wote.

Ban amesema ajenda hiyo inatoa msukumo mpya kwa ubia wa kimataifa, na kuweka msingi thabiti wa kutekeleza ajenda ya maendeleo baada ya 2015, na pia kutoa mwongozo kwa wadau kufanya uwekezaji busara kwa watu na sayari dunia unakohitajika,  unapohitajika na kwa kiwango kinachohitajika.

Mratibu wa kongamano hilo la Addis Ababa amekuwa ni Msaidizi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Idara ya masuala ya Kiuchumi na Kijamii katika Umoja wa Mataifa, Wu Hongbo:

(Sauti Wu Hongbo)

‘‘Ukiweka ajenda ya malengo endelevu  baada ya mwaka 2015 bila namna ya utekelezaji ni bure, kwahiyo kongamano  hili la ufadhili kwa maendeleo linatoa usaidizi  mkubwa kwa utekelezaji wa ajenda ya  maendeleo endelevu.