Simanzi yatawala wakati wa heshima za mwisho kwa askari wa Mali
Nchini Mali ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kumarisha utulivu MINUSMA pamoja na jumuiya za kimataifa zinaendelea na uimarishwaji wa amani kupitia makubaliano ya amani ili kumaliza mzozo nchini humo huku ukikumbana na changamoto mbalimbali.
Miongoni mwa changamoto hizo ni kuuliwa kwa walinda amani ambapo juma lililopita wengina sita kutoak Burkina Faso waliuwawa huku katika shambulio lingine huko Timbuktu askari wengine watano waliuwawa. Ungana Joseph Msami katika makala ifutayo