Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yawawezesha wakimbizi fedha za pango za nyumba

UNRWA yawawezesha wakimbizi fedha za pango za nyumba

Wakimbizi wa Kipalestina walioko ukanda wa Gaza wamepokea ruzuku kwa ajili ya pango la nyumba na fedha kwa ajili ya kuwanganisha tena na jamii kupitia benki limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNRWA kiasi cha dola milioni 1.46 kimetumika kwa ajili ya mpango huo unaotekelezwa kwa kipindi cha mwezi Septemba hadi Desemba 2014 ambapo familia za wakimbizi 2,499 zitanufaika na fedha hizo.

Shirika hilo linasema kuwa msaada wa kiasi cha dola 180,000 zilizotolewa juma hili zimewekwa kwa ajili ya ruzuku ya pango ya juma lililopita ili kutumika kwa ajili ya kipindi chae mwezi Septemba hadi Desemba 2014 na umewafikia familia 195.

UNRWA limeainisha pia kuwa malazi ya dharura, matengezo ya nyumba, na ujenzi ni kipaumbele cha shirika na kuongeza kuwa shirika linasalia katika ahadi yake ya usaidizi kwa familai athiriwa lakini bado linahitaji fedha ili kuendelea na mpango wa kutoa fedha tasilimu kwa ajili ya malazi.