Skip to main content

Uwekezaji katika ulinzi wa jamii una faida za moja kwa moja: FAO

Uwekezaji katika ulinzi wa jamii una faida za moja kwa moja: FAO

Ili kuhakikisha usalama wa chakula na lishe bora kwa njia endelevu ni lazima kuwekeza katika sekta ya umma, sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali. Hilo ni pendekezo la Shirika la chakula na kilimo duniani FAO, kandoni mwa kongamano la ufadhili kwa maendeleo linaloendelea mjini Addis Ababa.

Katika mahojiano na Idhaa hii, Mkurugenzi Mkuu wa FAO Jose Graziano Da Silva, amesema kwamba uwekezaji huo unapaswa kulenga uwekezaji katika elimu ya afya, mbinu za kuhifadhi, mifumo na unyunyuziaji maji kwa ajili ya kuimarisha ajira.

Bwana Da Silva amesema kwamba ni muhimu kuwekeza katika ulinzi wa jamii hususan maeneo ya vijijini, ambako asilimia 70 ya watu masikini zaidi wanaishi, ili kuhakikisha kwamba uzalishaji unaimarishwa akitoa mfano…..

Tuna watu takriban milioni 150 walioko chini ya  huduma ya ulinzi wa kijamii milioni 120 wakiwa Amerika Kusini ambako imedhihirika kwamba unapowapatia watu maskini zaidi fedha watazitumia kwenye lishe ambapo afya yao inaimarika na uzalishaji wao vile vile na hivyo kuna faida ya papo hapo.”