Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapinduzi ya mifumo ya takwimu kuchangia katika kutimiza maendeleo endelevu

Mapinduzi ya mifumo ya takwimu kuchangia katika kutimiza maendeleo endelevu

Ukusanyaji wa takwimu kwa kutumia mbinu za kisasa kama mfano simu za mkononi, GPS, kadi za benki au taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii ni muhimu katika kupanga, kufuatilia na kuimarisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

Hayo yameibuka wakati wa mkutano uliofanyika leo mjini Addis Ababa kwenye kongamano la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo linalohitimishwa hapo kesho.

Mtandao wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo Endelevu, UNSDN, umeshirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali, serikali na sekta binafsi katika kuzindua ubia kwa ajili ya kukusanya na kusambaza takwimu.

Mjadala huo umeongozwa na Maria Sarungi Tsehai, mwanaharakati wa mitandao ya kijamii aliyeanzisha alama ya reli au hashtag #ChangeTanzania kwenye Twitter. Anaeleza umuhimu wa mapinduzi ya takwimu.

(Sauti ya Maria)