Vijana wasaidiwe kujenga mustakhabali wa dunia: Ban
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka jumuiya ya kimataifa kusukuma usaidizi kwa vijana ili kuimarisha uwezo wao katika kusaidia mustakabali wa pamoja wa dunia. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte.
(TAARIFA YA PRISCIILA)
Katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya ujuzi kwa vijana inayoadhimishwa leo Julai 15 kwa mara ya kwanza, Bwana Ban amesema wakati kote duniani vijana wakiwa na fursa ya elimu kuliko siku za nyuma, bado vijana barubaru 75 milioni hawako shuleni hatua inayotishia upatikanaji wa ujuzi wanaohitaji.
Kwa upande wake mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana Ahmed Alhendawi ambaye yuko mjini Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo linalozungumzia uwekezaji kwa vijana anasema
(SAUTI AHMED)
‘‘Tutumie fursa hii kuu kufikiria uwekezaji mkubwa kwa kizazi hiki na kuwahusisha katika kufikiria sera zitakazo wawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi yao.’’
Akizungumzia fursa za ajira kwa vijana Ridhiwani Kikiwete ambaye ni kijana mbunge kutoka nchini Tanzania ameiambia iidhaa hii.
(SAUTI RIDHIWANI)