Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya Addis yalenga kuafikia ajenda ya kuchukua hatua

Mazungumzo ya Addis yalenga kuafikia ajenda ya kuchukua hatua

Huku mazungumzo ya faragha yakiendelea kwa siku ya pili mjini Addis Ababa kwenye kongamano la kimataifa kuhusu Ufadhili kwa Maendeleo, Kamati kuu itaanza kukutana leo usiku, kwa ajili ya majidiliano ya mwisho kuhusu azimio linalotakiwa kupitishwa na washiriki wa kongamano hilo. Azimio hilo linaloitwa Addis Ababa Action Agenda linatarajiwa kuonyesha msimamo wa nchi wanachama kuhusu udhibiti wa ulipaji ushuru.

 Margaret Novicki, msemaji wa Umoja wa Mataifa kwa kongamano hilo, amesema hayo kwa waandishi wa habari leo mjini Addis Ababa.

Akizungumza na idhaa hii katikati ya ukumbi wa kongamano baada ya mkutano na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa UNCTAD Mukhisa Kituyi amesema ana matumaini kwama nchi wanachama zitaafikia makubaliano ifikapo ukomo wa kongamano, alhamis hii.

(clip Kituyi)