Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio la kigaidi Cameroon

Ban alaani shambulio la kigaidi Cameroon

Katibu Mkuu amelaani vikali mashambulio mawili kwa pamoja kaskazini mwa Cameroon yaliyolenga mji uitwao Fotokol mnamo Julai 12 ambapo ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waathiriwa na serikali na watu wan chi hiyo.

Katika taarifa yake Ban amewatakia uponyaji wa haraka majeruhi kutokanana shambulio hilo la kigaidi na kuelezea kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali ya Cameroon katiak kukabiliana na Boko Haram wanaotuhumiwa kutekeleza shambulio hilo.

Kadhalika amepongeza nchi hiyo na watu wake  kwa kukaribish wakimbizi kutoka ukanda huo tangu kuanza kwa mzozo na kuelezea uungwaji mkono kutoka kwake sio tu kwa Cameroon bali pia kwa nchi za ukanda na kuchagiza ushirikiano zaidi katika kupambana na vitisho vya Boko Haram kwa kuzingatia sheria za kimataifa za usaidizi wa kibinadamu pamoja na haki za binadamu.