Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katazo la wakimbizi kutopiga kura CAR lifikiriwe upya: CAR

Katazo la wakimbizi kutopiga kura CAR lifikiriwe upya: CAR

Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi(UNHCR) limeitaka Jamahuri ya Afrika ya  Kati(CAR) kufikiria upya kuhusu  tangazo la kuwazuia mamia ya wakimbizi kupiga kura badaye mwaka huu ili amani timilifu irejee nchini humo.

Kwa mujibu wa afisa wa UNHCR Leo Dobbs, makataa hayo yameleta mshangao kwa wakimbizi hao ambao walikuwa wakijiandaa kushiriki uchaguzi.

(SAUTI LEO)

‘‘Wanahitaji kujenga imani kwa kuruhusu wakimbizi kupiga kura. Hiyo ni hatua katika kujenga imani ambayo itahamasisha wakimbizi, maridhiano na amani’’

Zaidi ya wakimbizi 400,000 wengi wao wakiwa Waislamu wamejihifadhi nje ya nchi kufuatia miaka kadhaa ya machafuko nchini CAR.