Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukuaji endelevu wa kiuchumi wahitaji kuwekeza katika usawa wa kijinsia

Ukuaji endelevu wa kiuchumi wahitaji kuwekeza katika usawa wa kijinsia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amesema jamii ya kimataifa haijawekeza ipasavyo katika usawa wa kijinsia, akiongeza kuwa upungufu huo wa fedha umekuwa kizuizi katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia.

Ban amesema hayo akihutubia mkutano maalum kuhusu maswala ya kijinsia uliofanyika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia wakati wa kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo.

Bwana Ban ameeleza kwamba ni asilimia 10 tu ya ufadhili wa kiserikali wa maendeleo ndio unalenga wanawake.Ameongeza kwamba hii inapaswa kubadilishwa ili kuweza kutimiza maendeleo na ukauaji wa uchumi ulio endelevu, jumuishi na sawa.

Katibu Mkuu amesema kwa upande mmoja serikali zinapaswa kuwekeza katika sera zinazopendekeza au kunufaisha zaidi wanawake na wasichana kwenye sekta ze elimu au kilimo.

Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo alikuwa Dkt. Musimbi Kanyoro kutoka Kenya , Rais wa Shirika la Global fund for Women

(Sauti ya Musimbi)