Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania, Ethiopia, Kenya na DRC nchi za kwanza kufaidika na mkakati mpya kwa wanawake na watoto

Tanzania, Ethiopia, Kenya na DRC nchi za kwanza kufaidika na mkakati mpya kwa wanawake na watoto

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezindua leo mkakati mpya wa kusitisha vifo vya wanawake wajawazito na watoto ifikapo mwaka 2030, uitwao mfuko wa ufadhili wa kimataifa, yaani Global Financing Facility, GFF.

Uzinduzi huo umefanyika kwenye mkutano maalum kuhusu wanawake na watoto, mjini Addis Ababa, huku nchi wanachama za Umoja wa Mataifa zikiendelea kujadiliana kuhusu ufadhili wa maendeleo.

Mkakati huo unalenga kuunganisha fedha kutoka serikali na sekta binafsi ili kuwekeza katika mifumo ya afya, chini ya uongozi za nchi zenyewe.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Bwana Ban amesema watoto ndio mtaji wa jamii kwa maendeleo ya baadaye .

Nchi nne zilizofadhiliwa katika hatua ya kwanza ya utekelezaji wa mkakati huo ulioanza mapema mwaka huu ni Ethiopia, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Tanzania.