Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha matangazo yakusitisha mapigano Colombia

Ban akaribisha matangazo yakusitisha mapigano Colombia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha matangazo yaliyotolewa hapo jana mjini Havana kuusu nia ya serikali ya Colombia na vikosi vya FARC-EP ya kuchukua hatua za kukomesha machafuko yanayoendelea nchini humo na kusongesha juhudiza majadiliano ili kufikika makubaliano ya amani haraka iwezekanavyo.

Bwana Ban katika taarifa yake pia amekaribisha pia adhma ya pande kinzani kukaraibisha Umoja wa Mataifa kusaidia majadiliano katika kamati ndogo ya kukomesha masuala ya mgogoro.

Amesisitiza utashi wa Umoja wa Mataifa katika kutoa usaidizi unaohitajika kuhakikisha majadiliano yanakamilika kwa mafanikio na utekelezaji  wa makubalainao ya amani ya Colombia.