Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko Iraq yaendelea kugharimu maisha ya maelfu:Ripoti

Machafuko Iraq yaendelea kugharimu maisha ya maelfu:Ripoti

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo inaonyesha kuwa machafuko nchini Iraq yanaendelea kusababisha maafa  kwa raia ambapo maelfu takribani raia wamuewawa huku takribani 30,000 wakijeruhiwa tangu mwezi January mwaka 2014.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI, kwa kushirikiana na ofisi ya kamishna wa haki za binadamu OHCHR ni ya kati ya kipindi cha Desemba 2014 hadi April 2015 ambapo inahusisha uchunguzi wa matukio na ushuhuda wa waathiriwa na mashahidi wakiwamo wakimbizi wa ndani.

Inaonyesha kuwa hali za raia katika maeneo yanayokaliwa na wapiganaji wanaotaka dola ya kiislamu  ISIL ni tete, wanaendelea kuuwawa mara nyingi hadharani hususani wanaopinga kundi hilo na kuinga mkono serikali  au vikosi vyake. Mbali na kuuwawa wengine wanatekwa nyara, huku wanahabari na madaktari wakilengwa.

Cecile Pouilly ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu

(SAUTI )

‘‘Ripoti hii inaainisha hali nchini Iraq katika kipindi cha miezi michache iliyopita. Inaonyesha hali mbaya kwa raia zaidi ya 15,000 waliouwawa tangu  Januari 2014. Uhalifu huu uliotendwa na ISIS uliorodheshwa kabla lakini sasa hali inasalia mbaya.’’

Ikigubikwa na matukio mengi yaliyo kinyume na haki za binadamu tripoti hiyo kadhalika imetuhumu vikosi vya jeshi la Iraq na washirika wake kwa mashambulizi ya angani na makombora na kusema kuwa vitendo hivi kwa ujumla sio tu kuwa vinavunja sheria za kimataifa bali pia  vyaweza kusababisha mauaji ya kimbari.