Sekta binafsi ni muhimu katika kufadhili maendeleo: UNCTAD

Sekta binafsi ni muhimu katika kufadhili maendeleo: UNCTAD

Dola trilioni 2.3 zitakosekana kila mwaka ifikapo 2030 ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu, amesema Katibu Mkuu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD, Mukhisa Kituyi.

Akihojiwa na Idhaa hii, Bwana Kituyi amesema hayo kabla ya kongamano la kimataifa kuhusu Ufadhili kwa Maendeleo utakaofanyika kuanzia jumatatu ijayo mjini Addis Ababa Ethiopia

(Sauti ya Kituyi )

Hata hivyo ameonya kwamba uwekezaji binafsi utachangia pakubwa katika maendeleo endelevu iwapo utadhibitiwa na sera thabiti, halikadhalika, iwapo serikali za nchi zinazoendelea zitawezesha ubunifu katika sekta mbalimbali.

Clip Kituyi 2