Ni mwanzo mzuri kwa usalama Libya: Ban

Ni mwanzo mzuri kwa usalama Libya: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefurahishwa na kuanza kwa makubaliano ya kisiasa ya Libya mjini Skhirat, nchini Morocco.

Katika taarifa yake kupitia msemaji wa Katibu Mkuu, Ban amesema anatarajia kukamilika kwa kasi kwa makubaliano hayo na utekelezaji wake akiongeza kuwa hio ni dhihirisho la utashi wa kisiasa na uthubutu unaoleta nchi hatua moja karibu zaidi katika kutatua tatizo la katiba na usalama.

Amekumbusha ahadi yake ya kuendelea kuwasaidia watu wa Libya kupitia mwakilishi wake maalum na ujumbe wa Umoaj wa Mataifa nchini humo (UNSMIL)