Skip to main content

Ban alaani shambulio la bomu nchini Chad

Ban alaani shambulio la bomu nchini Chad

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la bomu lililolenga soko mjini N'Djamena, nchini Chad hapo jana na kusababisha vifo vya watu 15 na kujeruhi kadhaa.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imemnukuu Bwana Ban akieleza rambirambi zake kwa familia za waathiriwa na serikali na watu wa Chad pamoja na kuwatakia uponyaji wa haraka majeruhi.

Amesema shambulio hilo la kufedhehesha dhidi ya raia katika mwezi huu wa mfungo wa Ramadan ni ukumbusho kwa kila mtu kuwa janga la ugaidi halina mipaka na kusisistiza umuhimu wa ushirikiano zaidi miongoni mwa nchi za ukanda.

Bwana Ban amesema ushirikiano huo unahitajika katika masuala ya misaada kibinadamu kimataifa, haki za binadamu na sheria za wakimbizi.