Skip to main content

Sekta ya huduma kuinua Afrika, UNCTAD yafungua ofisi Addis Ababa

Sekta ya huduma kuinua Afrika, UNCTAD yafungua ofisi Addis Ababa

Tarehe Tisa Julai mwaka huu, Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNCTAD lilizindua ripoti kuhusu uchumi barani Afrika! Jambo kubwa katika ripoti hiyo ni umuhimu wa sekta ya huduma katika kukwamua uchumi wa bara hilo ambalo kwa miongo zaidi ya mitano imekuwa ikipatia kipaumbele sekta ya viwanda na kilimo.

Je ni kwa kiasi gani sekta hiyo inaweza kuleta mabadiliko? Na ni harakati gani UNCTAD inachukua ili kubadili fikra hata za watendaji wa serikali za Afrika kubaini umuhimu wa kuweka sera sahihi ili kuchanusha sekta ya huduma badala ya kuachia sekta binafsi ikihaka peke yake? Assumpta Massoi alisaka kubaini hilo alipozungumza na Katibu Mkuu wa UNCTAD Dkt Mukhisa Kituyi wakati alipokuwepo New York, Marekani kushiriki vikao mbali mbali vya shirika hilo. Kwanza anaanza kwa kuelezea mambo waliyobaini.