Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maonyesho ya 'Saba Saba" Tanzania na jukwaa la wanawake la maendeleo!

Maonyesho ya 'Saba Saba" Tanzania na jukwaa la wanawake la maendeleo!

Wanawake, kila uchao harakati za kukwamua kundi hilo zinazidi kuimarika sambamba na lengo namba Tatu la maendeleo ya milenia yanayofikia ukomo mwezi Septemba mwaka huu. Lengo hilo linasaka usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake. Uwezeshaji unaozungumziwa ni ule wa kuweka fursa za kisheria na kisera ambazo kwazo wanawake wanaweza kushiriki katika shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii bila vikwazo. Nchini Tanzania harakati za kumkwamua mwanamke zinaimarika na zimekuwa dhahiri katika maonyesho ya kimataifa ya biashara al maarufu Saba Saba yanayofanyika jijini Dar es salaam. Je nini kimefanyika ungana na Assumpta Massoi katika makala hii.