Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi 1000 wawasili kwa siku Ugiriki: UNHCR

Wakimbizi 1000 wawasili kwa siku Ugiriki: UNHCR

Idadi ya wakimbizi wanaowasili katika visiwa nchiniUgiriki inaendelea kuongezeka ambapo hivi sasa wakimbizi 1000 kwa siku huwasili nchini humo limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR.

Kwa mujibu wa shirika hilo tangu kuanza kwa mwaka zaidi ya watu 70,000 wamewasili kwa njia ya bahari nchini humo ambapo asilimia 60 ya wakimbizi ni kutoka Syria wengine kutoka Afghanistan, Iraq, Eritrea na Somalia.

Hali hii inasababisha Ugiriki sasa kuwa na hali ya dharura ya wakimbizi mathalani jumanne wiki hii takribani wakimbizi 40 wakiwa katika boti iliyotokea Uturuki kuelekea Ugiriki ilipinduka katika moja ya visiwa na kuokolewa watu 19, miili mitano ya waliokufa imepatikana huku wengine 16 wakiwa hawajulikani walipo.

UNHCR imeonya kuwa idadi ya wasaka hifadhi nchini humo inaongezeka kwa kasi licha ya juhudi za mamlaka nchini humo,  imekuwa vugumu kukabiliana na wimbi hilo na hivyo kuhitaji

msaada kutoka barani Ulaya kabla hali haijawa mbaya zaidi.