Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutokomeza njaa kunahitaji ulinzi wa kijamii na uwekezaji unaowajali masikini- UM

Kutokomeza njaa kunahitaji ulinzi wa kijamii na uwekezaji unaowajali masikini- UM

Makadirio mapya ya Umoja wa Mataifa yameonyesha kuwa, kutokomeza njaa sugu kutahitaji kuwekeza dola 160 zaidi kila mwaka kwa kila mtu anayeishi katika umasikini uliokithiri, katika miaka 15 ijayo.

Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyoandaliwa na Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD na Shirika la Chakula Duniani, WFP, kutokomeza njaa duniani kwa njia endelevu ifikapo mwaka 2030, kutahitaji takriban dola bilioni 267 zaidi kila mwaka kwa wastani, kwa uwekezaji katika maeneo ya vijijini na mijini, na ulinzi wa kijamii.

Kwa kufanya hivyo, watu masikini watapata chakula na kuboresha maisha yao, kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyowasilishwa leo mjini Roma, Italia, kabla ya kuanza kwa kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo, mjini Addis Ababa Ethiopia, hapo Jumatatu, Julai 13.

Ripoti imesema pia kuwa, licha ya hatua zilizopigwa katika miongo michache iliyopita, watu milioni 800, hususan katika maeneo ya vijijini, hawana chakula cha kutosha.

Ertharin Cousin ni Mkurugenzi Mkuu wa WFP..

(SAUTI ETHARIN)