Kuwekeza Guinea, Sierra Leone na Liberia ni hatua sahihi kwa mustakhbal bora: Ban

10 Julai 2015

Mkutano wa kimataifa wa kujadili jinsi ya kukwamua nchi zilizokumbwa na mlipuko wa Ebola huko Afrika Magharibi umefanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo mwenyeji Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema mafanikio ya kudhibiti Ebola ni dhahiri lakini hakuna kulegeza Kamba. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Kazi iliyo mbele yetu ni kubwa na tunachopaswa kufanya ni kutimiza ahadi zetu ili kuhakikisha tunasaidia nchi zilizokumbwa na Ebola zitibu wagonjwa na zikwamuke!

Ni kauli ya Ban katika hotuba yake kwa washiriki wakiwemo Marais wa Guinea, Sierra Leone, Liberia na mwenyekiti wa Muungano wa Afrika, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe,akitanabaisha kuwa lengo kuu ni kujenga uwezo wa kuzuia majanga na kujenga uwezo wa kukabili kwa hiyo..

“Kuwekeza Guinea, Sierra Leone na Liberia kutatoa fursa ya manufaa ya kimataifa ya kuzuia milipuko midogo ya magonjwa eneo moja kuwa dharura za kitaifa au za kikanda. Na ndio maana leo ni zaidi ya hotuba na kutoa ahadi! Leo ni fursa ya kujenga ubia wa mustakbali bora wenye fursa nyingi na bila Ebola.”

Rais Mugabe akazungumza kwa niaba ya Muungano wa Afrika akisema..

(Sauti ya Mugabe)

“Licha ya mtazamo chanya kwa hivi karibuni, hebu nitoa hadhari kuwa hatupaswi kulegeza Kamba kwani masuala na udhaifu uliochochea mlipuko bado zipo na zinahitajika kushughulikiwa kwa kina.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter