Jukwaa mtandaoni latumika kuimarisha maisha ya wasichana Tanzania

Jukwaa mtandaoni latumika kuimarisha maisha ya wasichana Tanzania

Mafunzo kuhusu viongozi au watu wanaoenziwa kwa mchango wao kwa jamii ni muhimu hususan kama mbinu ya kuwapa changamoto watoto shuleni kama njia ya kuwezesha ndoto zao kwa ajili ya kuimarisha maisha ya kizazi kijacho. Ni kwa mantiki hiyo ambapo Shirika la Elimu, Sayansi na utamaduni UNESCO kwa kushirikiana na Camara Education inaendesha mradi wa kubadili maisha ya wasichana kupitia teknolojia barani Afrika.

Kulikoni? Ungana na Grace Kaneiya katika makala hii..