Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Nigeria imeazimia kutokomeza Boko Haram

Serikali ya Nigeria imeazimia kutokomeza Boko Haram

Serikali ya Nigeria imeonyesha azma mpya ya kutokomeza kikundi cha kigaidi cha Boko Haram, na hiyo ni kwa mujibu wa Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Afrika Magharibi, UNOWA, Mohammed Ibn Chambas.

Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa baada ya kuhutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, Bwana Chambas amesema..

(Sauti ya Chambas)

“Kilichodhihirisha sasa ni kwamba Boko Haram imekumbwa na makabiliano kwa kiasi fulani, ingawa bado hakijatokomezwa. Miundombinu yake imevunjwa nguvu, lakini bado ina uwezo wa kufanya mashambulizi ya kivita, ikiwemo ya kujilipua na mauaji ya kikatili ambayo tumeshuhudia.”

Amesema Umoja wa Mataifa tayari unashirikiana na nchi za  bonde la mto Chad katika kutokomeza Boko Haram kwa kusaidia uanzishwaji wa kikosi cha pamoja cha kukabiliana na kikundi hicho lakini akasema usaidizi zaidi unahitajika katika..

(Sauti ya Chambas)

“Kuwapatia msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi na wale ambao wamelazimika kukimbia makwao.”