Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio kuhusu mauaji ya kimbari ya Srebenica lagonga mwamba

Azimio kuhusu mauaji ya kimbari ya Srebenica lagonga mwamba

Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililolenga kulaani mauaji ya kimbari yaliyotokea miaka 20 iliyopita huko Srebrenica, nchini Bosnia na Herzegovina, limegonga mwamba baada ya Urusi kutumia kura yake turufu kupinga azimio hilo.

Katika upigaji kura nchi nne ambazo ni Angola, Venezuela, Nigeria na China hazikupiga kura kuonyesha msimamo wowote huku nchi Kumi zikiliunga mkono.

Hata hivyo kwa mujibu wa kanuni za Baraza la usalama azimio lolote ambalo litapigiwa kura hata moja ya hapana ya turufu litakuwa halijapitishwa.

Mapema kabla ya upigaji kura, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson akibutubia baraza amesema mauaji ya kimbari ya Srebrenica yamekuwa kipindi cha kusikitisha sana cha historia ya hivi karibuni, akieleza kwamba wakati ule Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa walishindwa kuzuia mauaji hayo.

Hata hivyo amesema kwa sasa hatua zimechukuliwa ili kuwezesha walinda amani kutumia nguvu za kijeshi ili kuhakikisha usalama wa raia.

Mwaka 1995, zaidi ya wanaume 8,000 na vijana barubaru waliuawa na waasi kutoka kundi la jeshi la Jamhuri ya Serbia lililoongozwa na Ratko Mladic ambaye sasa kesi yake iko ICC.

Nchi Nne ambazo zilipigia kura ya Ndiyo rasimu hiyo ya azimio iliyowasilishwa na Uingereza ni Chad, Chile, Jordan, Lithuania, Malaysia, New Zealand, Marekani, Hispania, Ufaransa na Uingereza.