Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini miaka Minne ya Uhuru bado shida na taabu: Ban

Sudan Kusini miaka Minne ya Uhuru bado shida na taabu: Ban

Miaka minne nikiwa Juba, Sudan Kusini nilishuhudia na raia wa nchi hiyo kupandishw kwa bendera ya taifa hilo change kabisa duniani, lakini matumaini  yao yametumbukia nyongo.

Ni ujumbe wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati huu ambapo Sudan Kusini inatimiza miaka minne tangu ipate uhuru wake baada ya kujitenga na Sudan.

Ban katika taarifa na msemaji wake amenukuliwa akisema baada ya uhuru na zaidi miezi 18 tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe maelfu ya raia wamesalia wakimbizi ndani ya nchi yao huku wengine wakisaka hifadhi nchi jirani.

Ametoa wito kwa Rais Salva Kiir na makamu wake wa zamani Riyek Machar na pande nyingine kwenye mzozo huo kutambua kuwa vita si suluhu bali suluhisho la kisiasa ndio muarobaini.

Kwa mantiki hiyo amewataka viongozi hao kudhihirisha uongozi wao kwa kuwekeza katika suluhu la kisiasa litakalowezesha kupatikana kwa makubaliano thabiti ya amani huku akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua kusaidia kumalizwa kwa vita hivyo.

Ban pamoja na kushuruku watoa huduma za misada katika mazingira hatari, amesema Umoja wa Mataifa kwa upande wake utaendelea kusaidia kupatikana kwa suluhu la kisiasa sambamba na kuwapatia misaada ya kibinadamu na ulinzi raia walio hatarini.