Mradi wa IFAD wabadilisha maisha ya familia 20,000 Uganda
Nchini Uganda, mradi wa majaribio umesaidia kubadilisha maisha ya watu masikini zaidi, kwa kutumia njia bunifu inayowasaidia kuwa na taswira tofauti ya maisha yao, huku ukiwapa stadi na ujuzi wa kujiondoa katika umasikini. Ungana na Joshua Mmali, akihadithia kuhusu jinsi mradi huo wa Shirika la Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD, unavyosaidia kuwainua watu kutoka umasikini