Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Stadi kupitia mradi wa ILO zaboresha maisha ya vijana Tanzania

Stadi kupitia mradi wa ILO zaboresha maisha ya vijana Tanzania

Nchini Tanzania mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na shirika la kazi duniani, ILO kupitia  mradi wa ujasiriamali kwa vijana umeimarisha stadi za biashara kwa vijana ikiwemo wachora sanaa na hivyo kuinua mapato yao.

Hayo yamedhihirika katika maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea jijini Dar es salaam, ambako mmoja wa wanufaika Amos Mtambala  akiwa kwenye banda la Umoja wa Mataifa, amemweleza Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja huo kuwa kupitia mradi huo wanafundishwa jinsi ya kuanzisha biashara, kuikuza na hata kuanzisha mpya iwapo ya awali imemchosha na sasa anashuhudia mafanikio..

(Sauti ya Amos-1)