Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Warundi zaidi wakimbilia Uganda

Warundi zaidi wakimbilia Uganda

Hali ya usalama inayoendelea kuzua shaka nchini Burundi wakati uchaguzi wa Rais ukisubiriwa,  inawamiminisha zaidi raia wake katika nchi jirani ikiwemo Uganda ambako zaidi ya wakimbizi 200 wanapokewa kila siku. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Tayari mzozo wa kisiasa umesababisha zaidi ya wakimbizi 150,000 kusaka usalama katika nchi jirani za Tanzania, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zamiba tangu Novemba mwaka jana.

Kati ya wakimbiziz hao, Uganda imepokea zaidi ya 10,300 ambao wanasimulia kwamba wanavutiwa na sera za serikali zilizo rafiki kwa wakimbizi kulingana na taarifa wanazopata kutoka wenzao waliowatangulia.

Charles Yaxley Msemaji wa UNHCR Uganda amesema, wanatafuta ufadhili wa dola milioni 205 za Kimarekani kama uitikio wa kibinadamu kwa warundi wote wanaokimbilia nchi jirani.

(Sauti ya Charles Yaxley)

 “Fedha zaidi zinahitajika kwa dharura za kushughulikia mahitaji ya kibinadamu ya Warundi laki mbili wanaotarajiwa kuwa wamekimbia nchi hiyo ifikapo mwishoni mwa Septemba”

Wanaowasili Uganda wanadai kusumbuliwa na wanamgambo na maafisa wa polisi kwenye vizuizi vya barabarani katika safari yao ya karibu kilomita 500 kwa wale wanaokimbia kutoka mji mkuu Bujumbura.