Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa uwekezaji wa sekta binafsi maziwa makuu Afrika kufanyika Mwakani

Mkutano wa uwekezaji wa sekta binafsi maziwa makuu Afrika kufanyika Mwakani

Mkutano wa uwekezaji wa sekta binafsi kwenye ukanda wa maziwa makuu utafanyika tarehe 24 na 25 mwezi Februari mwakani huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Mkutano huo unafanyika kwa mujibu wa makubaliano ya amani, usalama na ushirikiano ya ukanda huo, PSCF ambapo utaleta pamoja wawekezaji wa sekta binafsi, maafisa wa serikali na wafanyabiashara na wenye viwanda kujadili fursa mbali mbali za biashara.

Halikadhalika wataweza kutathmini mazingira ya biashara na kuidhinisha uwekezaji kwenye miradi mbali mbali itakayoidhinishwa.

Kikao cha maandalizi kilifanyika Kinshasa, washiriki wakiwa ni pamoja na mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye maziwa makuu Said Djinnit na Katibu Mtendaji wa mkutano wa maziwa makuu Balozi Vicente Muanda.

Viongozi hao wamesema ni mkutano huo utakaofanyika wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu tangu kutiwa saini kwa PSCF, ni fursa ya kuweka mazingira bora ya biashara kushamiri na kuondoa machungu ya mamilioni ya wakazi wa ukanda huo.

Wamesema ni vyema kukumbuka kuwa ukanda wa maziwa makuu ni eneo ambalo kwalo wakazi wake wengi wanasoma na ni vijana wa mijini ambao na wanahitaji usaidizi.