Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatoa wito uhai wa raia uheshimiwe Yemen

UNHCR yatoa wito uhai wa raia uheshimiwe Yemen

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR limerejelea wito wake kwa pande kinzani katika mzozo wa Yemen ziheshimu uhai wa raia, kufuatia shambulizi la roketi mwishoni mwa wiki dhidi ya shule ya malezi mjini Aden, ambalo lilisababisha vifo vya wakimbizi 12.

Usiku wa Jumamosi Julai 4, roketi ilivurumishwa kwenye shule ya malezi ya Al Tadamon mjini Aden, ikapenya kuta kadhaa na kuwaua wakimbizi 12, wakiwemo Wasomali 11 na raia mmoja wa Ethipoia. Watano miongoni mwao walikuwa watoto.

Wakimbizi wengine 12 walijeruhiwa na kupelekwa hospitalini. Watu wengine kutoka familia kadhaa walikuwa wamelala wakati wa shambulizi hilo, na kwa bahati nzuri, hawakujeruhiwa.