Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yapata msaada wa kukabiliana na ukatili wa kijinsia, CAR

IOM yapata msaada wa kukabiliana na ukatili wa kijinsia, CAR

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM  limepokea msaada wa zaidi ya dola Laki Saba za kimarekani kutoka serikali ya Canada kwa ajili ya kusaidia juhudi za shirika hilo za kupambana na ukatili wa kingono na kijinsia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR). Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Msemaji wa IOM Geneva, Uswisi Joel Millman amesema msaada huo ambao umetolewa kupitia mradi wa Canada wa Ufadhili wa Kimataifa wa Amani na Usalama (GPSF) utasaidia zaidi wanawake na wasichana walioathiriwa na mzozo wakiwemo wale wanaorejea makwao.

Amesema ukiwa ni mwaka moja na nusu ya tangu kuibuka kwa mzozo nchini  Jamhuri ya Kati (CAR), ubakaji na aina nyingine za ukatili wa kijinsia vimesalia kuwa tishio kubwa zaidi kwa usalama wa wanawake na wasichana waliojikuta katika mzozo wa hivi karibuni, ambao umelazimisha takribani watu 900,000 kukimbia makwao.

Kwa sasa wanaendelea kusaka ulinzi na msaada kwenye sehemu mbalimbali za nchi hiyo. Joel Millman ni msemani wa IOM Geneva, Uswisi.